Mola wenu Mlezi anakujueni vilivyo. Akipenda atakurehemuni, na akipenda atakuadhibuni. Na hatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mola wenu Anawajua nyinyi zaidi, enyi watu, Akitaka Atawarehemu Awaafikie kwenye Imani au Akitaka atawafisha kwenye ukafiri kisha Awaadhibu. Na hatukukutumiliza, ewe Mtume, uwe ni muwakilishi juu yao, unayapanga mambo yao na unawalipa kwa matendo yao, jukumu lako ni kuyafikisha uliyotumilizwa kwayo na kuieleza njia iliyolingana sawa.